[dropcap]K[/dropcap]wanza kabisa Fun-Lugha si shule ya kujifunzia lugha. Hatuna madarasa hapa kwetu na kila kitu kwa sasa kinafanyika mtandaoni na ila atakayetaka kuonana nasi tuko tayari kufanya hivyo popote atakapopenda.
Kikubwa tunachofanya hapa Fun-Lugha ni kuwaunganisha watoaji huduma za lugha (mfano walimu, wakalimani n.k) pamoja na wateja wao. Wote wawili wanatulipa kiasi kidogo cha fedha ambacho hulipwa mara moja tu, yaani kwa mfano mwalimu na mwanafunzi hawatahitaji kutulipa kila wanapokuwa na darasa. Walimu wa lugha hufundisha kwa wakati wao, sehemu watakayoelewana na wanafunzi wao na hata bei zao wataelewana na wanafunzi. Sisi kwa kweli hatuwezi kujua bei ya mwalimu labda awe ameonyesha kwenye wasifu wake unaopatikana hapa hapa kwenye tovuti yetu chini ya All Service Providers
Kwa bei za watoa huduma wengine tuulize sisi kwani zitategemeana na uzito wa kazi. Kwa watoa huduma wanaohitaji kujisajili na Fun-Lugha tunaomba mtuandikie kupitia hapa Kwa wateja wanaohitaji huduma zetu pia mtuandikie kupitia hapa Kwa maswali au maelezo zaidi kuhusu chochote kingine kile tuandikieni kupitia hapa